1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Ruanda yaisifu Canada kwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari

20 Oktoba 2005

Waziri wa sheria nchini Ruanda, Eda Mukabagwiza, amesema Ruanda imefurahishwa na hatua ya polisi nchini Canada kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 nchini Ruanda anayeishi mjini Toronto.

Muendesha mashataka nchini Ruanda, Emmanuel Rukangira, aliyeshirikiana na maofisa katika uchunguzi, amesema Desire Munyaneza mwenye umri wa miaka 39 amekamatwa kwa mashtaka saba ya mauji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.

Waziri Mukabagwiza amesema maofisa wa Canada hawatakubali kuwaachilia wahalifu wa mauji hayo ya kimbari kujificha nchini humo. Amesema bado kuna matafia kadhaa yanayowaficha washukiwa wa maujai hayo na kuyataka yaige mfano wa Canada.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW