1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kigali: Rwanda yakaribisha kusalim amri kamada wa waasi Rais wa Rwanda ...

19 Novemba 2003

jana alikaribisha kusalim amri kiongozi wa waasi wa Kihutu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, akisema ni mfano kwa waasi wengine waliojificha msituni katika tifa hilo kubwa barani Afrika. Paul Rwarakabije, kamanda wa jeshi la FDLR lenye makao yake nchini Congo, alisalim amri mbele ya serikali ya Rwanda inayotawaliwa na Watutsi jumamosi iliyopita. Chama cha FDLR, ambacho wanachama wake waliowengi ni Wahutu kutoka Rwanda, kimekadiriwa na wachambuzi kuwa na wapiganaji wa chini kwa chini 15,000 hadi 20,000, wanaoendesha vita vya kuipindua serikali ya Rwanda kutoka vituo vyao vya msituni mashariki mwa Congo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW