1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Tume yaundwa kuhusu mauaji ya mashahidi

22 Desemba 2003

Baraza la Seneti nchini Rwanda limeanzisha tume maalum ya uchunguzi wa taarifa za karibuni kuhusu mfululizo wa mauaji ya mashahidi mbali mbali wa vitendo vya ukatili na mauaji ya kuangamiza jamii yaliofanyika mwaka wa 1994. Kiongozi wa tume hiyo mpya ambae ni Seneta Antoine MUGESERA amesema kuwa Baraza limeamua kuunda tume hiyo yenye wajumne 5 baada ya kupata taarifa za matukio hayo. Jumatatu iliopita, chama kikuu cha wahanga wa mauaji hayo ya 1994 kinachoitwa IBUKA kilitoa taarifa yenye kulaani mauaji ya mashahidi 3 yaliofanyika karibuni katika mkoa wa kusini magharibi wa Gikongoro. Chama hicho kilionya kuwa mauaji hayo ni sehemu ya kampeni ya unyanyasaji, utishaji na mauaji ya kiholela inayoendelea sehemu mbali mbali za Rwanda kwa nia ya kujaribu kuwazuwia mashahidi wa mauaji hayo ya 1994 kujieleza katika kesi zinazohusiana na vitendo hivyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW