1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Waandishi wa habari watiwa nguvuni

21 Novemba 2003

Idara za polisi nchini Rwanda, zimewakamata waandishi wa habari wa tatu, kwa tuhuma za kutangaza habari za uongo, na ambazo zinachochea chuki za kikabila.

Taarifa iliyotangazwa na shirika la habari AFP, likinukulu msemaji wa polisi ya Rwanda, Bwana Damas Gatare, inasema Mkurugenzi wa Gazeti la kujitegemea Umuseso, Bwana Robert Sebufurira, na waandishi habari wengine wawili wa gazeti hilo, Charles Kabonero, na Emmanuel Niyonteze, wametiwa nguvuni.

Shirika la habari AFP linasema kwa mujibu wa mashirika ya kutetea haki za binaadamu nchini Rwanda, waandishi wa habari watano wamekamatwa.

Gazeti Umuseso ndilo gazeti pekee la kujitegemea nchini Rwanda, lisilofungamana na idara za serikali, wala za chama tawala Rwandese Patriotic Front, na waandishi wake wamekua wakikamatwa mara kwa mara, wakishtumiwa na idara za usalama kupigia debe wapinzani, na kuchochea chuki za kikabila.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW