1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI. Wafungwa elfu 36 waachiliwa huru

30 Julai 2005

Maelfu ya wafungwa wameachiliwa huru kutoka jela nchini Rwanda katika mpango wa kupunguza msongamano magerezani.

Mnamo siku ya jumatano wiki hii baraza la mawaziri nchini Rwanda liliidhinisha hoja ya kuachiliwa huru wafungwa elfu 36 kutoka magereza 16 nchini humo.

Wengi wa wafungwa walioachiwa huru wamekiri kuhusika na mauaji ya kinyama ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Milolongo ya magari makubwa inawapeleka waachiliwa hao katika kambi za mafunzo wanakotarajiwa kujifunza juu ya haki na maridhiano kwa muda wa mwezi mmoja kabla ya kurudi vijijini mwao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW