1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI: Wafungwa wa Ruanda walioachiliwa huru mwezi uliopita warudi nyumbani leo

29 Agosti 2005

Wafungwa wengi kati ya wafungwa elfu 22 walioachuiliwa huru nchini Ruanda mwezi uliopita wameruhusiwa kwenda makwao hii leo baada ya vituo walikokuwa wakipokea mafunzo ya kuwajumulisha katika jamii kufungwa.

Wafungwa hao ambao karibu wote walishtakiwa kwa kuhusika katika mauaji ya halaiki ya mwaka wa 1994, walipokea mafunzo maalumu kuhakikisha mauaji ya aina hiyo hayatokei tena nchini humo.

Naibu wa mwanasheria mkuu nchini Ruanda, Martin Nyoga, amethibitisha kwamba wafungwa hao wameanza safari zao kurudi nyumbani lakini akasema bado anasubiri idadi yao kamili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW