1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI-Wananchi wa Rwanda waanza wiki ya kumbukumbu ya maji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyoua watu laki

7 Aprili 2005

Wananchi wa Rwanda leo wameanza wiki ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari,yaliyoangamiza maisha ya watu wanaofikia laki nane mwaka 1994.

Kiasi cha watu 5,000 walikusanyika katika mji wa kaskazini-mashariki wa Murambi,ambapo Rais wa nchi hiyo Paul Kagame,aliongoza kumbukumbu hiyo ya miaka 11,ambapo siku 100 zilishuhudia mauaji ya kikatili kwa watu kuchinjwa kati ya mwezi wa Aprili hadi Julai mwaka 1994.

Rais Paul Kagame akizindua wiki hiyo ya maombolezo,alitoa heshima zake na kumuenzi Baba Mtakatifu Yohanna Paulo wa pili,kwa kumueleza alikuwa ni mtu wa amani na maridhiano.

Baba Mtakatifu aliyefariki dunia siku ya Jumamosi iliyopita,alikuwa kiongozi wa kwanza wa kimataifa kukemea mauaji ya kimbari ya Rwanda,yakiwemo yale yaliyofanywa na Wakatoliki na kuonya kuwa wote waliohusika na mauaji hayo watakabiliana na adhabu mbele ya Mungu na pia sheria za hapa duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW