1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI-Wiki ya maadhimisho ya mauaji ya kimbari ya anza nchini Rwanda.

7 Aprili 2005

Wananchi wa Rwanda wameanza wiki ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini humo miaka 11 iliyopita,ambapo pamoja na mambo mengine,mabaki ya waliouawa katika mauaji hayo yatafukuliwa kutoka makaburi ya pamoja na kuzikwa tena katika eneo maalum.

Ingawa inaonekana shughuli hiyo ya kuzika upya mabaki hayo ikapooza machungu kwa baadhi ya familia za watu zaidi ya laki nane waliouawa,bado nchi ya Rwanda ipo katika hekaheka za kuendesha kesi za wale waliohusika na mauaji hayo,huku Wanyarwanda wengi wakiwa wanalaani mauaji hayo.

Wiki iliyopita kikundi kikuu cha waasi wa Kihutu,ambacho kinahusishwa na mauaji hayo kwa kiasi kikubwa,kililaani mauaji hayo kwa mara ya kwanza na kusema kuwa kinaachana na mapambano ya mtutu wa bunduki kutokea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Nao wafungwa wanaohusishwa na mauaji hayo chini ya mahakama za Umoja wa Mataifa,wametoa taarifa ya kuadhimisha mauaji hayo kwa sala na kufunga.

Maadhimisho ya mwaka huu yanaonekana yatagubikwa na kunyosheana vidole kati ya Rwanda na Ufaransa,huku Rwanda ikiishutumu Ufaransa kuhusika na mauaji ya mwaka 1994 kwa kutoa mafunzo kwa wanamgambo wa Intarahamwe wanaohusishwa na mauaji ya watutsi waliowengi pamoja na Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW