1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI Wolfowitz ziarani Ruanda

16 Juni 2005

Rais wa benki ya dunia, Paul Wolfowitz, akiwa ziarani nchini Ruanda, ameomba msamaha kwa ulimwengu kushindwa kuingilia kati kuyazuia mauaji ya halaiki nchini humo. Amesema jamii ya kimataifa inatakiwa kuchukua dhamana kwa mauaji hayo.

Ijapo hakuna mambo mengi yanayoweza kufanywa kwa wakati huu, Wolfowitz anafikiri ni muhimu kufanya juhudi zaidi badala ya kuomba msamaha. Yumo nchini Ruanda katika awamu ya tatu ya zaira yake barani Afrika kama rais wa benki ya dunia.

Tayari amezitembela Nigeria na Burkina Faso, ambako alizungmzia juu ya ruzuku inayotolewa na mataifa ya magharibi kwa wakulima wa pamba. Hapo kesho ataondoka Kigali kwenda Afrika Kusini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW