1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI:18 wahukumiwa vifungo virefu gerezani

3 Desemba 2003
Mahkama ya Rwanda imewahukumu wanaume 18 vifungo vya muda mrefu gerezani kwa kushiriki katika mauaji ya takriban Watutsi 20,000 hapo mwaka 1994. Watu hao 18 wanatuhumiwa kwa kusimamia mauaji yaliofanywa na wanamgambo wa Kihutu pamoja na raia kwa Watutsi hao waliokuwa katika hifadhi ya jengo la kanisa huko Nyarubuye. Mmojawapo wa watuhumiwa hao 19 alihukumiwa kifungo cha miaka 25 geerezani,16 walihukumiwa vifungo ya miaka 16 gerezani kwa kila mmoja, mwengine mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka 7 na mmoja aliachiliwa huru. Watu hao 18 waliwaongoza wanamgambo wa Kihutu na raia ambao walilishambulia kanisa la Nyarubuye hapo April 15 mwaka 1994 na baadae kundi hilo likarudi siku ya pili yake kwenda kuwamaliza wale walionusurika. Takriban Watutsi milioni moja na Wahutu wenye msimamo wa wastani inasemekana kuwa waliuwawa nchini Rwanda kati ya mwezi wa April na July mwaka 1994.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW