1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIGALI:Waasi wa Kihutu wa Rwanda wawauwa watu 13 Kongo

23 Julai 2005

Waasi wa kihutu nchini Rwanda wameripotiwa kuwauwa raia wasiopungua 13 huko mashariki mwa jamhuri ya kidemkrasi ya Kongo.

Kwa mujibu wa Gavana mtendaji wa mkoa wa Kivu kusini waasi hao ni wanachama wa Demokratic Forces for Liberation of Rwanda na wamekuwa wakifanya operesheni zao katika eneo la mashariki ya Kongo katika kipindi cha miaka 11 iliyopita.

Serikali ya Kigali imewalaumu waasi hao kwa kuhusika kwenye mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994 .

Wiki iliyopita waasi waliwachoma moto hadi kufa watu 39 kwenye kijiji kimoja walichokivamia huko Kivu Kusini.

Umoja wa wa Mataifa umeanzisha operesheni kadhaa katika eneo hilo mwezi huu kuwasaka waasi hao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW