1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiir amfuta uwaziri mke wa Machar

4 Machi 2023

Rais wa Sudan Kusini amewafuta kazi mawaziri wake wawili, akiwemo waziri wa ulinzi ambaye pia ni mke wa mpinzani wake mkubwa wa kisiasa wa muda mrefu, Riek Machar, katika hatua inayohofiwa kuurejesha mpya mpasuko wao.

Salva Kiir Mayardit | sudanesischer Präsident
Picha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Ofisi ya Machar ilisema siku ya Jumamosi (Machi 4) kwamba hatua ya Rais Salva Kiir ya kumfuta kazi Waziri Angelina Teny ilichukuliwa bila kuwepo mashauriano.

Salva Kiir alimfuta pia kazi waziri wa mambo ya ndani kutoka chama chake bila kutoa maelezo zaidi. 

Soma zaidi: Mgogoro bado unaendelea kuitikisa Sudan Kusini

Papa Francis akamilisha ziara yake nchini Sudan Kusini na amehimiza juu ya kukomeshwa chuki na ghasia.

Msemaji wa Riek Machar, Puok Both Baluang, alibainisha katika chapisho la Facebook kuwa hatua ya rais ni ukiukaji wa makubaliano.

Kwa mujibu wa masharti ya mkataba wa amani wa mwaka 2018 uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano, wizara ya ulinzi inatakiwa kuongozwa na chama cha Machar huku wizara ya mambo ya ndani ikiongozwa na mjumbe kutoka chama Kiir.