1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Kijana aua na kujeruhi wanafunzi kwa risasi, Iowa

5 Januari 2024

Kijana mmoja wa miaka 17 amemuua mwanafunzi mmoja wa darasa la sita na kuwajeruhi wengine watano baada ya kuwafayatulia risasi wanafunzi waliokuwa wakirejea shuleni baada ya likizo ya majira ya baridi.

Kijana wa miaka 17 aua mwanafunzi kwa risasi, Iowa
Watu wakiondoka katika jengo la McCreary baada ya kukutanishwa na watoto wao baada ya shambulizi la risasi katika shule ya Perry Januari 4, 2024Picha: Charlie Neibergall/AP Photo/picture alliance

Maafisa wamesema mtuhumiwa huyo Dylan Butler, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya upili ya Perry aliwafyatulia risasi wanafunzi wa shule ya Iowa, na baadae alikutwa amekufa kutokana na jeraha la risasi.

Tukio hilo lililotokea siku ya kwanza ya kufungua shule huko Iwoa ni sehemu ya janga la kitaifa la machafuko ya kutumia silaha mashuleni ambayo yameongezeka katika miaka ya karibuni.

Soma pia:Biden aomboleza mauaji ya kutumia bunduki huko Texas

Mkurugenzi msaidizi wa idara ya kuchunguza uhalifu ya jimbo Mitch Mortvedt amesema Butler alituma machapisho kadhaa mtandaoni kabla ya tukio hilo, ingawa amesema uchunguzi bado unaendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW