1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Kijana wa Kiisraeli apatikana amekufa Ukingo wa Magharibi

13 Aprili 2024

Jeshi la Israel na polisi ya nchi hiyo wamesema mwili wa kijana wa Kiisraeli ambaye yumkini aliuawa kwenye shambulio lililofanywa na Wapalestina umepatikana hii leo huko Ukingo wa Magharibi.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel Picha: Ohad Zwigenberg/AFP/Getty Images

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 14 alipotea jana Ijumaa na mamlaka za Israel zimeyaelezea mauaji yake kuwa "shambilizi la kigaidi". Kisa hicho huenda kitaongeza machafuko kwenye eneo hilo, ambayo hivi sasa tayari yamefikia viwango cha kutisha.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel amesema washambuliaji waliohusika watapatikana na ametaka raia wa nchi hiyo kutovizuia vyombo vya usalama kutimiza kazi yao.

Hapo jana, wakati vikosi vya Israel vilifanya operesheni ya kumtafuta kijana huyo, na walowezi wa Kiyahudi walikivamia kijiji kimoja cha Wapalestina, na kuchoma moto nyumba na magari.

Mtu mmoja aliuawa kwenye vurumai hiyo lakini haikufahamika iwapo alipigwa risasi na vikosi vya Israel au walowezi waliojihami kwa bunduki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW