Kijana wa miaka 20 ashitakiwa kwa ushoga Uganda
28 Agosti 2023Kulingana na hati ya mashitaka iliyoonekana na shirika la habari la Reuters, kijana huyo alishitakiwa Agosti 18 kwa kosa la kushiriki mapenzi ya jinsia moja na mwanamme mwenzake mwenye umri wa miaka 41.
Hata hivyo, hati hiyo haikufafanua ni kwa nini kitendo hicho kilichukuliwa kuwa ni kibaya.
Soma zaidi:Benki ya Dunia yakemea sheria ya Uganda dhidi ya mashoga
UN: Uganda lazima ifute sheria yake mpya ya kupinga ushoga
Kwa kuwa kosa lenye adhabu ya kifo husikilizwa Mahakama Kuu pekee, mshitakiwa huyo alisomewa mashitaka na kurudishwa rumande, kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Jacqueline Okui, aliyezungumza na Reuters.
Wakili wa mshukiwa huyo, Justine Balya, alisema anaamini kwamba sheria hiyo nzima inakwenda kinyume na katiba.