1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kijiji kimoja chashambuliwa kaskazini mwa Beirut

25 Septemba 2024

Mashambulizi yameelekezwa kwenye kijiji kimoja katika eneo la milimani kaskazini mwa Beirut kwa mara ya kwanza kulingana na wakazi wa eneo hilo, huku vyombo vya habari vya serikali vikiripoti mashambulizi ya makombora.

Lebanon | Beirut
Shambulizi la Israel mjini BeirutPicha: Hassan Ammar/dpa/AP/picture alliance

Mashambulizi yameelekezwa kwenye kijiji kimoja katika eneo la milimani kaskazini mwa Beirut kwa mara ya kwanza kulingana na wakazi wa eneo hilo,  huku vyombo vya habari vya serikali vikiripoti mashambulizi ya makombora na Israel ikisema inafanya mashambulizi makubwa dhidi ya ngome za kundi la Hezbollah.

Soma: Idadi ya waliouwawa Lebanon yavuka 550, Kamanda mwingine wa Hezbollah auwawa Beirut

Shirika la habari la kitaifa la Lebanon limeripoti kuwa makombora mawili yalianguka katika kijiji cha Maaysra" chenye idadi kubwa ya jamii ya Washia kwenye eneo lenye Wakristo wengi kilichoko umbali wa kilomita 25 kutoka Beirut. Wakaazi wamethibitisha kuwa shambulizi hilo lililenga kijiji chao, na kuharibu nyumba na mgahawa.

Wakati huo huo, Kundi la Hezbollah limerusha komborakuelekea Tel Aviv mapema leo katika shambulizi lake la ndani kabisa ndani ya Israeli, na kuashiria kuongezeka kwa mapigano kati ya pande hizo mbili baada ya shambulizi la Israeli dhidi ya Lebanon kusababisha vifo vya mamia ya watu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW