1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Bunge la China lafungua kikao chake cha kila mwaka

5 Machi 2024

Bunge la China limefungua kikao chake cha kila mwaka kwa hotuba ya Waziri Mkuu wa taifa hilo, Li Qiang, iliyotoa tathmini ya kazi za serikali katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita na mwelekeo kwa mwaka mmoja unaokuja.

Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, akituhubia Bunge la nchi hiyo.
Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, akituhubia Bunge la nchi hiyo.Picha: Florence Lo/REUTERS

Kikao hicho kinachofanyika kwenye eneo linalofahamika kama "Ukumbi wa Umma wa China" katikati mwa mji mkuu Beijing, kikihudhuriwa na maelfu ya wawakilishi wa kuchaguliwa kutoka kila pembe ya taifa hilo.

Kwenye hotuba yake Waziri Mkuu Qiang amesema China inalenga kufikia ukuaji uchumi wa asilimia 5 mwaka huu kupitia mpango wa mageuzi kwenye sekta za maendeleo pamoja na kupunguza matumizi holela ya serikali za mitaa.

Ama kuhusu suala la Taiwan, Qiang, amesema Beijing itakuwa imara kuelekea kutimiza dhamira ya kuuungana tena na kisiwa hicho  chenye utawala wake wa ndani, ambacho kimekuwa kitovu cha mvutano kati ya China na hasimu wake Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW