1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Kikosi kipya cha Kenya chenye Polisi 230 chawasili Haiti

9 Desemba 2025

Polisi 230 wa Kenya wamewasili Haiti Jumatatu jioni, kikiwa ni kikosi cha kwanza cha kigeni tangu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipoidhinisha kutanua kikosi kilichopo na kinachopambana na magenge ya uhalifu.

Port-au-Prince I Kikosi cha Kenya kikiwasili Haiti kukabiliana na magenge ya wahalifu
Kikosi cha Kenya kikiwasili katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince ili kukabiliana na magenge ya wahalifuPicha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Msemaji wa kikosi hicho Jack Ombaka ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa kikosi hicho kimeimarishwa kuanzia mwezi Februari mwaka huu na kwamba kwa sasa kina jumla ya mafisa wapatao 980 huku idadi iliyokuwa ikitarajiwa awali ikiwa ni maafisa 2,500.

Kenya ndio imetuma maafisa wengi zaidi lakini Jamaica, Bahamas, Belize, Guatemala na El Salvador pia zimetuma askari. Magenge ya uhalifu nchini Haiti  yamekuwa yakiendesha mauaji, ubakaji na uporaji, katika mzozo mkubwa uliopelekea takriban watu milioni 1.4 kuyakimbia makazi yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW