Kikosi cha kulinda amani Haiti chaahidi kuleta utulivu
9 Julai 2024Kamanda huyo wa kikosi cha askari wa Kenya,Godfrey Otunge amesema Ujumbe huo unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa uko tayari kuhakikisha chaguzi za kidemokrasia zinafanyika katika taifa hilo la Carribean.
"Tunakazi tuliyojitolea kuifanya.Na kwahivyo tunapswa kuifanya kwa viwango vya ubora kadri ya uwezo wetu na kuleta mafanikio. Kazi yetu ni kuhakikisha tunarudisha amani kote nchini Haiti.''
Soma pia:Polisi wa Kenya waendelea kuwasili Haiti kuyadhibiti magenge
Ni mara ya kwanza kwa jeshi la polisi la Kenya lililoko Haiti kutowa tamko kwa umma,kupitia mkutano na waandishi habari uliooneshwa kwenye kituo cha habari cha taifa, nchini Haiti.
Kikosi cha askari wa Kenya kinatarajia kuungana baadae na askari kutoka Bahamas,Bangladesh,Barbados,Benin,Chad na Jamaica katika harakati za kuyakabili magenge ya Haiti.