1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Kikosi cha pili cha polisi kuwasili Haiti wiki chache zijazo

Sylvia Mwehozi
3 Julai 2024

Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille amesema kikosi cha pili cha ujumbe wa polisi wa kimataifa unaoongozwa na Kenya nchini humo kitawasili ndani ya wiki chache zijazo.

Kenia | UN Friedensmission in Haiti
Rais wa Kenya William Ruto akiwaaga maafisa wa polisi wanaolekea HaitiPicha: REBECCA NDUKU/PRESIDENTIAL COMMUNICATION SERVICE/EPA

Conille ameyasema hayo wakati wa ziara yake mjini Washington ambako alikutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken.

Kundi la kwanza la maafisa wa polisi 200 wa Kenya, ambao ni sehemu ya ujumbe ulioidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, waliwasili Haiti mwezi uliopita.

Soma pia: Rais Ruto wa Kenya asisitiza kupeleka polisi nchini Haiti wiki chache zijazo

Kikosi hicho kinalenga kusaidia polisi wa Haiti kuleta utulivu nchini humo, ambapo magenge ya kihalifu yanadhibiti takriban asilimia 80 ya mji mkuu.

Haiti, kwa muda mrefu imekuwa ikikumbwa na ghasia, lakini hali ilizidi kuwa mbaya zaidi mwishoni mwa Februari wakati makundi yenye silaha yalipoanzisha mashambulizi katika mji mkuu wa Port-au-Prince.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW