Kikosi cha RSF chadai jeshi la Sudan limeshambulia Khartoum
15 Mei 2023Matangazo
Taarifa iliyotolewa na kikosi hicho cha RSF imesema leo kwamba mashambulizi hayo "yaliua na kuwajeruhi mamia ya watu wasiokuwa na hatia."
Hata hivyo, madai hayo ya mashambulizi bado hayajathibitishwa na taasisi ya kujitegemea, ingawa baadhi ya mashuhuda wameandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa mashambulizi hayo yalitokea mapema mwezi huu.
Mashambulizi yaendelea Khartoum wakati wapinzani wakikutana Saudia
Shirika la misaada la CARE limetahadharisha kuwa mzozo huo unaweza kulemaza sekta ya afya hasa katika mji mkuu, Khartoum, ambako karibu theluthi mbili ya vituo vya afya bado vimefungwa - kimoja tu kati ya vituo sita vya afya ndicho kinachofanya kazi kwa sasa.