1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kila Upande Wadai Ushindi wa Uchaguzi wa Rais

Oumilkher Hamidou23 Desemba 2013

Mgombea wa kambi iliyoko madarakani,Hery Rajaonarimpianina anasema ana hakika ya kuibuka na ushindi wa uchaguzi wa rais nchini Madagascar ambao wasimamizi wa kimataifa wanasema ulikuwa huru na wa kuaminika.

Mgombea wa upande wa serikali,Hery RajaonarimampianinaPicha: Reuters

"Hesabu zinaonyesha,mie ndie mshindi,hakuna ubishi,nimeshinda,hata kama kweli bado matokeo rasmi hayajatolewa,tunazungumzia mkondo na kutokana na makadirio mie ndie nilieshinda" amesema Rajaonarimampianina mbele ya maripota wa shirika la habari la Ufaransa-AFP.

Matokeo ya awali ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais,zikihesabiwa kura kutoka asili mia 15 ya vituo vya uchaguzi,yanampatia mgombea huyo wa upande wa serikali,asili mia 53.6 ya kura.

Mpinzani wake Robinson Jean Louis,mgombea wa rais wa zamani Marc Ravalomanana amelaani"udanganyifu mkubwa" akihoji wakati huo huo yeye ndiye mshindi-wafuasi wake wamemhakikishia anasema amejikingia asili mia 65 ya kura.Hapo awali alikadiria kujikingia asili mia 56 ya kura.Jean Louis alitaka bila ya kufanikiwa hapo jana matokeo ya uchaguzi yasitangazwe akilalamika dhidi ya kile alichokiita "visa vya udanganyifu vilivyolengwa kumuibia ushindi."

Uchaguzi wa Kuaminika na wa Uwazi

Hata hivyo wasimamizi wa kimataifa wakiwemo wale wa Umoja wa ulaya hawakuthibitisha hadi wakati huu ripoti kuhusu visa vya udangayifu.

Mgombea wa upánde wqa rais wa zamani Richradson Jean LouisPicha: picture-alliance/dpa

"Kwa mtazamo wa Umoja wa Ulaya,uchaguzi ulikuwa wa kuaminika,huru na wa uwazi" amesema mkuu wa tume ya wasimamizi ya Umoja wa ulaya Maria Muniz de Urquiza.

Amewatolea wito wagombea wa pande zote mbili wajizuwie na kuheshimu utaratibu wa uchaguzi.

"Ni kawaida kwa mgombea aliyekosa kura alizokuwa akitarajia kuzungumzia kuhusu "udanganyifu" amesema msimamizi mmoja wa kigeni wakati wa mkutano na waandishi habari mjini Antananarivo.

"Uchaguzi umepita katika hali ambayo wapiga kura walipata nafasi kuwachagua bila ya pingamizi wagombea wao" alisema hapo awali rais wa zamani wa kisiwa cha Mauricious,Cassam Uteem anaeongoza tume ya wasimamizi kutoka taasisi ya upigaji kura kwaajili ya demokrasia ya kudumu barani Afrika-EISA yenye makao yake makuu mjini Johannesburg.Hakuna sababu yoyote ya kuamini kama kumefanyika udanganyifu -ameongeza kusema.Maoni sawa na hayo yametolewa pia na mwakilishi wa Umoja wa mataifa nchini Madagascar Fatouma Samoura.

Waliopiga Kura ni Wachache tu

Uchaguzi wa rais na bunge unaangaliwa kama hatua ya mwanzo muhimu itakayokitoa kisiwa hicho cha bahari ya Hindi katika mgogoro mkubwa wa kisiasa,kiuchumi na kijamii tangu miaka karibu mitano iliyopita.

Wapiga kura wakisubiri zamu yaoPicha: Reuters

Wasimamizi wamesikitishwa hata hivyo na idadi ndogo tu ya wapiga kura walioteremka vituoni kupiga kura:asili mia 48.tu ya wapiga kura milioni 7.9.

Mwadishi:Hamidou Oummilkheir/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu