1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Kilicho nyuma ya vita vinavyosababisha njaa Sudan

30 Agosti 2024

Mzozo wa Sudan uliozuka Aprili 2023 umesababisha wimbi la ghasia za kikabila, na kuibua mzozo mkubwa zaidi wa wakimbizi wa ndani ulimwenguni, na kusababisha mzozo wa chakula hasa katika jimbo la Darful.

Sudan | Mzozo | Raisa wakikimbia mapigano
Raia wa Sudan wakikimbia mapigano kuelekea sehemu salamaPicha: LUIS TATO/AFP

Kwanza kuna swali la msingi ambalo wengi wanajiuliza ambao wameanza kufuatilia mzozo huu kwa siku za karibuni, swali hilo ni nini hasa kilichosababisha mapigano hayo? Mvutano ulikuwa ukiongezeka kwa miezi kadhaa kabla ya mapigano.

Kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Wanamgambo wa RSF kuripuka katika mji mkuu Khartoum mwezi Aprili 15, 2023. Jeshi na RSF walikuwa katika ushirikiano tete baada ya kuipindua serikali ya kiraia katika mapinduzi ya Oktoba 2021, hatua

ambayo ilizuia mabadiliko kutoka kwa utawala wa kiimla wa Omar al Bashir. Bashir aliondolewa mamlakanai mwaka 2019.

Mabishano kati ya pande hizo mbili yalivunja mpango unaoungwa mkono kimataifa ambao ungezindua mpango mpya wa mpito na vyama vya kiraia.

Soma pia:Mkuu wa jeshi la Sudan asema hatoshiriki mazungumzo ya amani Uswisi

Jeshi na RSF  kila upande ulitakiwa kuchukua madaraka chini ya mpango huo na maeneo mawili yalionekana kuwa na utata.

Moja ilikuwa ratiba kwa RSF kuunganishwa katika vikosi vya kawaida vya jeshi na pili ilikuwa mtiririko wa utoaji wa amri kati ya jeshi na viongozi wa RSF na suala la uangalizi wa raia.

Lakini pande hizo zinazozozana zimekuwa katika ushindani wa maslahi ya biashara, ambayo walikuwa wanatafuta kuyalinda.

Washiriki wakuu kwenye mzozo huo?

Wahusika wakuu katika mzozo wa madaraka ni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, mkuu wa jeshi na kiongozi wa baraza tawala la Sudan tangu 2019, na naibu wake wa zamani kwenye baraza, kiongozi wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti.

Ufafanuzi: Je ni nchi zipi zinahusishwa na vita vya Sudan?

01:48

This browser does not support the video element.

Hemedti, ambaye alikua tajiri kupitia madini ya dhahabu na biashara nyingine anaongoza RSF.

Washiriki wa familia yake na ukoo wana majukumu makubwa na nguvu za kijeshi huko katika eneo la magharibi la Darfur, ambapo RSF iliibuka kutoka kwa wanamgambo waliopigana bega kwa bega na wanajeshi wa serikali kuwaangamiza waasi katika vita vya kikatili ambayo ilizuka kwa ukali baada ya 2003.

Soma pia:WFP yawachunguza maafisa wake nchini Sudan kwa ulaghai

Wachambuzi wanasema msimamo wa Burhan hauna uhakika, kwa wafuasi wa Bashir wanaoegemea kwenye itikadi kali na maveterani wa vita ambao  wamekuwa wakipata nguvu tangu mapinduzi ya 2021.

RSF inasema inapigania kuondoa mabaki ya utawala wa Bashir, wakati jeshi linasema linajaribu kuilinda serikali dhidi ya waasi "wahalifu".

Mashuhuda wanasema RSF na washirika wao wamekuwa wakifanya vitendo vibaya kabisa vyenye kutweza utu, ikiwemo mauwaji ya kikabila, unyanyasaji wa kingono na uporaji.

Wakaazi wamelishutumu jeshi kwa mauaji ya raia katika mashambulizi ya kiholela na mashambulizi ya anga. Pande zote mbili kwa kiasi kikubwa wamekanusha tuhuma dhidi yao.

Ushindi unatarajiwa kwenye mzozo?

Ingawaje jeshi la Sudan lilianzisha vita kwa rasilimali za hali ya juu. pamoja na silaha za ya anga, RSF iliyotambuliwa rasmi 2017 imekuwa na nguvu katika katika miaka ya hivi karibuni na kuwa jeshi lenye vifaa vya kutosha katika maeneo yote ya Sudan.

Katika siku za kwanza za vita, vitengo mahiri zaidi vya RSF vilifanikiwa kuingia katika vitongoji vya mji mkuu.

Kuelekea mwishoni mwa 2023, RSF ilifanya maendeleo ya haraka ili kuimarisha nguvu zake huko Darfur na kuchukua jimbo la El Gezira kusini mwa Khartoum, eneo muhimu katika sekta ya kilimo.

Soma pia:Blinken aelezea matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita Sudan

Lakini kwa upande wake jeshi lilipata nguvu tena na maendeleo katika eneo la  Omdurman mwezi Machi, mojawapo ya miji mitatu inayounda mji mkuu, lakini baadae RSF ilipata mafanikio tena katika Majimbo ya White Nile na Gedaref.

Mzozo huo umekuwa chachu ya mashindano kwa mataifa yenye ushawishi kwa Sudan, ikiwemo kikanda na mataifa mengine makubwa ya  ndani ya bara la Afrika na nje likiwemo Marekani,  Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Misri, Ethiopia, Iran na Urusi.

Vurugu zauwa watu 38 El-Fashir Sudan

01:16

This browser does not support the video element.