Licha ya ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, wakulima wa Makuweni nchini Kenya wana njia za kukabiliana na hali hiyo na kujizalishia chakula cha kutosha. Katika vidio hii, mkulima anazungumzia jitihada za kuchanganya mbinu za kale na sasa katika kilimo, zikiwemo za uhifadhi wa maji ya mvua, upandikizaji miche na udhibiti wa wadudu wanaoharibu mazao, bila kutumia kemikali za sumu.