Kilman asema mkataba wa usalama na Australia kupitiwa upya
5 Septemba 2023Mvutano huo ulisababisha kuanguka kwa serikali ya mtangulizi wake.
Akizungumza siku moja baada ya kuchaguliwa na wabunge kushika wadhifa huo, Kilman amesema mkataba uliotiwa saini baina ya Vanuatu na Australia mnamo Disemba mwaka jana unahitaji kutizamwa tena kwa sababu haitokuwa rahisi kuridhiwa na bunge bila ya kuwepo mabadiliko.
Kilman aliingia madarakani jana baada ya wabunge kuiangusha serikali ya waziri mkuu Ishmael Kalsakau wakimtwika dhima kwa kutia saini mkataba huo wanaosema unaiweka rehani hadhi ya "kutoegemea upande wowote" ya kisiwa cha Vanuatu.
Wanasiasa wa nchi hiyo wanaamini vilevile mkataba huo unatishia kuinyima Vanuatu misaada kutoka China katika wakati mataifa ya magharibi ya kiongozwa na Marekani yanajaribu kuzuia kutanuka kwa nguvu na ushawishi wa Beijing kwenye kanda ya Pasifiki.