1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Satelaiti ya ujasusi ya Korea Kaskazini tayari kuzinduliwa

19 Aprili 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa nchi yake imetengeneza satelaiti ya kwanza ya ujasusi wa kijeshi, na kwamba anapanga kuizindua siku ambayo haikuwekwa wazi.

Nordkorea Kim Jong Un mit Tochter
Picha: KCNA/AFP

Majaribio ya siku za nyuma yameonyesha kuwa nchi hiyo inao uwezo wa kupeleka satelaiti angani, lakini wataalamu wanatilia shaka ikiwa inao utaalamu wa kuunda kamera zenye ufanisi wa kiwango cha ujasusi, ikizingatiwa kuwa picha zilizotokana na majaribio ya awali hazikuwa na ubora wa kuridhisha.

Soma pia:Korea Kaskazini yafanya jaribio la chombo kinachoweza kushambulia chini ya bahari

Akitembelea kituo cha utafiti wa anga za mbali cha nchi yake, Kim alinukuliwa na shirika la habari la serikali, KCNA, akisema kuwa satelaiti yenye uwezo wa kufanya ujasusi wa kijeshi ni muhimu kwa nchi yake kuweza kutumia makombora yake maalumu kwa kubeba vichwa vya nyuklia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW