1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kim Jong Un aapa kuendelea kuimarisha uwezo wa nyuklia

13 Julai 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema nchi yake itaendelea kuimarisha uwezo wake wa kupigana kwa kutumia silaha za nyuklia.

Nordkorea | Kim Jong Un besucht militärische Satellitenstation
Picha: KCNA/REUTERS

Kim ameyasema hayo wakati aliposimamia majaribio ya pili ya kombora jipya la masafa maarefu linaloweza kuilenga Marekani kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali vya Korea Kaskazini vilivyoripoti hii leo Alhamisi.  

Soma zaidi: Marekani, Korea Kusini zakanusha kuingia anga la Korea Kaskazini
Korea Kaskazini yaahidi kuunga mkono kikamilifu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

Korea Kusini, Japan na Marekani zimeilaani Korea Kaskazini kwa uzinduzi huo zikisema ni tishio kwa amani ya kanda na kimataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepanga kukutana siku ya Ijumaa (Julai 14) kuijadili hatua ya Korea Kaskazini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW