1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Kim Jong Un afungua mkutano wa kisiasa kuhusu kilimo

Hawa Bihoga
27 Februari 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amefungua mkutano mkubwa wa kisiasa ukibebba agenda ya kilimo, huku tathmini za nje zikionesha nchi hiyo ya Asia Mashariki inakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.

Nordkorea Kim Jong Un
Picha: KCNA VIA KNS/AFP

Wataalamu wa Korea Kusini wanakadiria kuwa Korea Kaskazini inaupungufu wa takriban tani milioni moja za nafaka.

Hii ikiwa ni asilimia ishirini ya mahitaji yake ya kila mwaka baada ya janga la Uviko-19 kutatiza kilimo na uagizaji kutoka China.

Korea Kaskazini yaonyesha silaha zake katika gwaride

Ripoti za hivi karibuni ambazo hazikuthibitishwa zimesema idadi isiojulikana na Wakorea kaskazini wamekufa kwa njaa.

Lakini waangalizi hawajaona dalili zozote za vifo vya watu wengi au njaa nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW