Kim Jong Un ajivunia mafanikio ya jeshi la nchi yake
12 Desemba 2025
Kim amekuwa akiongoza mikutano muhimu wiki hii ili kujadili mipango ya sera na namna ya kuitekeleza, wakati nchi hiyo inapojiandaa kwa mkutano wa tisa wa chama cha Wafanyakazi cha Korea, unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka ujao.
Shirika la Habari la serikali KCNA limeripoti kuwa, kiongozi huyo ameeleza umuhimu wa Korea Kaskazini kujitegemea zaidi na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Katika hatua nyingine, Kim Jong Un na Rais wa Urusi Vladimir Putin wamesaini mkataba wa pamoja wa ulinzi huku Korea Kaskazini ikiripotiwa kutuma wanajeshi wake katika uwanja wa vita kuisaidia Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.
Inaripotiwa kuwa Korea Kaskazini inapokea msaada wa kifedha, teknolojia ya kijeshi, pamoja na nishati kutoka Moscow kama malipo kwa hatua yake kutuma wanajeshi kuisaidia Urusi.