1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un akutana na Waziri wa maliasili wa Urusi

19 Novemba 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekutana Jumatatu na waziri wa maliasili wa Urusi Alexander Kozlov.

Kim Jong Un akisalimiana na waziri wa maliasili wa Urusi Alexander Kozlov
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akisalimiana na waziri wa maliasili wa Urusi Alexander Kozlov.Picha: Korean Central News Agency/Korea News Service/AP/picture alliance

Hii inachukuliwa kama ishara ya hivi punde ya kuimarika kwa mahusiano kati ya Pyongyang na Moscow. Wakati wa mkutano huo, Kim amesema kuna ulazima wa kutanua ushirikiano katika sekta ya biashara, sayansi na teknolojia, kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa nchi hizo mbili.

Soma pia: Korea Kaskazini yaidhinisha mkataba wa kihistoria wa ulinzi na Urusi

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, amezitaka Urusi na Korea Kaskazini kukomesha ushirikiano wao wa kijeshi ambao ameutaja kuwa haramu. Kwa upande wake Pyongyang imekosoa ushirikiano wa pande tatu kati ya Korea Kusini, Marekani na Japan na kusema unasababisha hali ya mifarakano na makabiliano.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW