1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kim Jong Un atangaza vifaa vya kimkakati kwa jeshi la anga

Saleh Mwanamilongo
30 Novemba 2025

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ametangaza kuwa jeshi la anga la nchi hiyo litapewa "vifaa vipya vya kijeshi vya kimkakati".

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: Korean Central News Agency/AP Photo/picture alliance

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, ametangaza kuwa jeshi la anga la nchi hiyo litapewa "vifaa vipya vya kijeshi vya kimkakati". 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali katika ripoti zake za Jumapili, Kim alitoa kauli hiyo Ijumaa katika maadhimisho ya miaka 80 ya jeshi la anga, akiwa na binti yake Ju Ae, anayechukuliwa kuwa mrithi wake.

Bila kutoa maelezo zaidi, Kim alisema jeshi la anga litakuwa na jukumu jipya la kukabiliana na ujasusi na uchokozi wa kijeshi kutoka kwa maadui.

Picha za serikali zilionyesha Kim na Ju Ae wakitazama ndege za kivita zikifanya mazoezi angani. Hatua hii inakuja wakati mazungumzo ya kijeshi yaliyopendekezwa na Korea Kusini yamekataliwa na Pyongyang, huku mvutano wa mpakani ukiongezeka na Seoul ikionya hatari ya kutokea kwa mapigano ya bahati mbaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW