1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kim Jong Un ayaamuru majeshi yake kwa ajili ya mashambulizi

Zainab Aziz Mhariri: Mohammed Khelef
10 Mei 2019

Kiongozi wa Korea Kaskazini ameliamrisha jeshi lake kuimarisha nguvu ya mashambulizi huku akiagiza kurushwa kombora jingine wakati ambapo mivutano imeongezeka.

USA | Präsident Donald Trump
Picha: Reuters/K. Lamarque

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametoa amri hiyo baada ya kupatikana habari kwamba Marekani imeikamata meli kubwa ya mizigo ya Korea Kaskazini. Marekani imesema imeitwaa meli hiyo kwa ilikuwa inasafirisha shehena ya makaa ya mawe kinyume cha sheria. Kim ameyataka majeshi yake yajiweke tayari kwa mapambano.

Wizara ya sheria ya Marekani imesema meli hiyo ya tani,17,061 inayoitwa Wise Honest ndiyo kubwa kabisa ya Korea Kaskazini ambayo kwanza ilizuiwa na Indonesia mwaka uliopita na sasa imekamatwa na Marekani.

Mivutano imejitokeza katika muktadha wa mkwamo wa mazungumzo baina ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini na Rais wa Marekani Donald Trump. Mazungumzo baina ya viongozi hao wawili yalimalizika  bila ya kufikiwa mapatano walipokutana kwa mara ya pili nchini Vietnam.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: picture-allianvce/AP Photo/Korean Central News Agency

Kim Jong Un aliitaka Marekani iondoe vikwazo iliyvoiwekea nchi yake na upande wake RaisTrump  aliitaka Korea Kaskazini iondoe silaha zake za nyuklia. Hata hivyo Rais Trump na mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in wamesema majaribio hayo mapya hayasaidii  lakini wameeleza kuwa mazungumzo hayatavunjika. Hata hivyoJapan imesema Korea Kaskazini imekiuka maazimio ya Umoja  wa Mataifa yanayopiga marufuku majaribo ya makombora ya masafa marefu. Naibu wa katibu wa baraza la mawaziri nchini Japan Kotaro Nogami amesema:

Japan ambayo imo katika umbali wa kuweza kushambuliwa na makombora ya masafa mafupi ya Korea Kaskazini, wakati wote imekuwa inatetea vikali maazimio madhubuti dhidi ya Korea Kaskazini ili kuilamizisha nchi hiyo iachane na makombora hayo ya masafa mafupi na  pia iachane na mpango wa silaha za nyuklia.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya bunge la Korea Kusini amewaambia waandishi habari kwamba wataalamu wa kijeshi wa Korea Kusini na wa Marekani wanafanya tathmini ya majaribio yaliyofanywa na Korea Kaskazini ili kubainisha iwapo yalikuwa makombora aina ya Iskander yanayotengezwa na Urusi.

China imesema haina habari za kutosha juu ya jaribio lililofanywa na Korea Kaskazini. Badala yake imezitaka Marekani na Korea Kaskazini zijizatiti kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo sambamba na kuendeleza kasi ya kupunguza mivutano kwenye rasi ya Korea. 

Vyanzo: RTRE/APE

 

  

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW