1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kim kutembelea kiwanda cha kuunda ndege za kivita Urusi

Sylvia Mwehozi
15 Septemba 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amewasili leo katika mji wa Komsomolsk-on-Amur ulioko nje kidogo mashariki mwa Urusi.

Russland, Tsiolkovsky | Nordkoreas Machthaber Kim Jong-Un
Picha: KCNA/KNS/AP/picture alliance

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amewasili leo katika mji wa Komsomolsk-on-Amur ulioko nje kidogo mashariki mwa Urusi. Kiongozi huyo anatarajiwa kukitembelea kiwanda kinachotengeneza ndege za kivita na vifaa vingine. Shirika la habari la Urusi TASS, limeripoti kwamba kiwanda hicho kinaunda ndege za kisasa za kivita za Urusi.

Hapo jana Kim, akiwa ameongozana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, alikitembelea kituo cha safari za anga za mbali cha  Vostochny Cosmodrome.Rais Putin akubali mwaliko wa Kim Jong Un

Korea Kusini na Marekani zimeelezea wasiwasi wake kwamba ziara ya Kim inalenga kupanua ushirikiano wa kijeshi katika kile kinachoweza kuwa ni makubaliano ya kubadilishana silaha na teknolojia. Washington na Seoul zinadai kuwa Korea Kaskazini huenda ikiipatia silaha Moscow huku nayo ikinufaika na teknolojia za hali ya juu zinazohusiana na satelaiti za kijasusi za kijeshi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW