1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamaica

Kimbunga Beryl chahama kuelekea Houston

8 Julai 2024

Kimbunga Beryl huenda kikafika ngazi ya pili ya ukubwa katika kipimo kinachotumiwa kupanga kitisho cha vimbunga wakati kitakapotua katika eneo la Houston

Mexiko Hurrikan Beryl
Picha: Fernando Llano/AP Photo/picture alliance

Siku ya Jumapili, kimbunga Beryl kilitarajiwa kuimarika na kufikia ngazi ya kwanza ya ukubwa katika kipimo kinachotumiwa kupanga kitisho cha vimbunga kiliposafiri juu ya maji yenye joto. NHC imetoa tahadhari za vimbunga katika sehemu kubwa ya pwani ya Texas.

Watabiri wa hali ya hewa waonya kuhusu athari za kimbunga Beryl

Watabiri wa hali ya hewa wanaonya kuwa Beryl inaweza kusababisha upepo mkali na mvua katika pwani ya Texas na kwingineko.

Soma pia:Kimbunga Beryl chaipiga Jamaika na sasa kinaelekea Mexico

Tayari maeneo ya pwani jana yalikuwa yanashuhudia kuongezeka kwa vina vya maji ya bahari na maafisa wa kaunti waliamuru kuhamishwa kwa watu kutoka mji mmoja wa ufuo wa bahari.

Soma pia:Kimbunga Beryl chaipiga Jamaika

Walinzi wa Pwani ya Marekani, jana alasiri walifunga bandari ya Houston kutokana na kuongezeka kwa hali mbaya ya bahari. Pia walifunga bandari za mji wa Texas, Freeport na Galveston huko Texas.