1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Dennis chaelekea Marekani

10 Julai 2005

Miami:

Kimbunga cha Dennis leo kimekusanya nguvu zake tena baada ya kuleta madhara makubwa Cuba na Haiti. Kimbunga hicho sasa kinaelekea katika pwani za Marekani ambazo mwaka wa jana zimeathiriwa na gharika. Watu wapatao zaidi ya millioni moja wameariwa kuondoka katika maeneo ambayo huenda yakakumbwa na kimbunga nchini Marekani ambacho kimewaua watu 15 katika Karibiki. Wakazi wa Key West nchini Marekani wamepumua baada ya kimbunga Dennis kutopita katika eneo lao na kuelekea Florida. Miji ya Marekani, ambayo huenda ikashambuliwa na kimbunga cha Dennis ni Mississippi, Alabama na magharibi mwa Florida.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW