1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Kimbunga Ditwah chasababisha vifo vya watu 123 Sri Lanka

29 Novemba 2025

Sri Lanka imeomba msaada wa kimataifa leo wakati idadi ya vifo vilivyotokana na mvua kubwa na mafuriko yaliyochochewa na kimbunga Ditwah, ikipanda na kufikia 123.

Sri Lanka Wilaya ya Kandy 2025 | Maporomoko ya ardhi na maafa baada ya mvua kubwa kunyesha Sri Lanka
Athari za kimbunga Ditwah wilaya ya kandy nchini Sri LankaPicha: jiayang samila/Xinhua/IMAGO

Sri Lanka imeomba msaada wa kimataifa leo wakati idadi ya vifo vilivyotokana na mvua kubwa na mafuriko yaliyochochewa na kimbunga Ditwah, ikipanda na kufikia 123 huku watu wengine 130 hawajulikani walipo. Kituo cha kudhibiti maafa nchini humo DMC, kimesema mfumo mbaya wa hali ya hewa umeharibu nyumba zipatazo 15,000 na kusababisha watu karibu alfu 44,000 kupelekwa kwenye makazi ya muda ya serikali. 

Mkurugenzi Mkuu Sampath Kotuwegoda amesema shughuli za kutoa misaada zimeimarishwa kwa kutumwa maelfu ya wanajeshi kutoka vitengo tofati vya jeshi, likiwemo la wanamaji na jeshi la anga.

Kimbunga Ditwah kinaonekana kuondoka kisiwani leo Jumamosi na kinaelekea nchi jirani ya India upande wa kaskazini, lakini kimesababisha uharibifu mkubwa, ikiwemo maporomoko mapya ya udongo katika wilaya ya kati ya Kandy iliyoko kilometa 115 kutoka mji wa Colombo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW