1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMsumbiji

Kimbunga Freddy kupiga tena Msumbiji

10 Machi 2023

Kimbunga Freddy kinatarajiwa kulikumba eneo la pwani ya kusini mwa Afrika kesho Jumamosi, baada ya kusababisha vifo vya watu takribani 21 nchini Msumbiji na Madagascar wakati kilipopiga mwezi uliopita.

Mosambik I Strum Freddy in Inhambane
Picha: Luciano da Conceição/DW

Shirika la kukabiliana na majanga la Msumbiji limesema kuwa zaidi ya watu 166,000 waliathiriwa wakati kimbunga hicho kilipoikumba kusini mwa Msumbiji wiki mbili zilizopita, na mafuriko kuharibu barabara, nyumba na shule.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kiutu, OCHA, imesema watu wapatao 565,000 wako katika hatari katika majimbo ya Zambezia, tete, Sofala na Nampula, huku jimbo la Zambezia likitarajiwa kuathiriwa zaidi.

Kimbunga Freddy  kitasababisha mvua kubwa Msumbiji pamoja na kusini mwa Malawi. Shirika la Hali ya Hewa Duniani, WMO limesema huenda likaanzisha uchunguzi baada ya kimbunga hicho kutoweka, ili kubaini iwapo kilivunja rekodi hiyo kwa muda mrefu zaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW