1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Kimbunga Khanun chaelekea Korea Kusini, Japan

7 Agosti 2023

Korea Kusini na Japan zimo kwenye tahadhari wakati Kimbunga Khanun kikitarajiwa kuyapiga maeneo kadhaa ya mataifa hayo mawili, baada ya kusababisha madhara ikiwemo vifo kilipowasili kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.

Satellitenaufnahme - Sturm über Brasilien
Picha: NASA/AFP

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Japan imesema kimbunga hicho kinatazamiwa kuleta mvua kubwa kwenye mkoa wa Kyushu, baada ya kulipiga eneo la Okinawa na kusababisha vifo vya watu wawiii, kujeruhi wengine 100 na kuharibu miundombinu.

Wasiwasi wa kutokea madhara makubwa umewalazimisha maafisa wa mji wa Nagasaki, moja ya miji ya mkoa wa Kyushu, kupunguza ukubwa wa shughuli za kila mwaka za kuwakumbuka waliopoteza maisha kwenye shambulizi la bomu la nyuklia kwenye mji huo la mwaka 1945.

Soma zaidi: Kimbunga Doksuri chawahamisha maelfu China
China yatoa tahadhari ya mvua kubwa mjini Beijing

Nchini Korea Kusini, mamlaka tayari zinajiandaa kuwahamisha maelfu ya skauti waliokusanyika kwa kongamano la kimataifa kusini magharibi wa nchi hiyo. 

Mamia ya mabasi yametumwa kuwaondoa karibu skauti 36,000 kutoka nchi 156 duniani kutokana na mashaka kuwa eneo wanapokutana litakumbwa na kishindo cha Kimbunga Khanun.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW