1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiTaiwan

Kimbunga Kong-rey chapiga Taiwan

31 Oktoba 2024

Kimbunga kikali, Kong-rey kimepiga Alhamisi kwenye pwani ya mashariki ya Taiwan huku miji yote na kaunti zikitangaza siku ya mapumziko.

Taiwan | Ankunft des Taifuns «Kong-rey» im Nordosten Taiwans
Picha: Johnson Lai/AP/dpa/picture alliance

Dhoruba kubwa zaidi kwa ukubwa kutokea katika kipindi cha miaka 30. Kulingana na kituo kikuu cha kusimamia masuala ya hali ya hewa cha Taiwan, kimbunga hicho kilipiga kaunti yenye milima ya Taitung yenye wakazi wachache, huku upepo mkali na mvua kubwa ikiathiri karibu kisiwa chote.

Kituo hicho cha hali ya hewa kimesema kimbunga hicho kitakuwa kikubwa zaidi kupiga kisiwa hicho tangu mwaka 1996.

Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, rais wa nchini hiyo Lai Ching-te, amesema anatumai kila mtu nchini humo atashirikiana katika kuepusha majanga na pia kujiepusha na mienendo hatari kama vile kutazama mawimbi wakati wa kimbunga.