1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Milton chaacha uharibifu mkubwa Florida

10 Oktoba 2024

Kimbunga Milton kimetuwa jimboni Florida na kusahabisha uharibifu mkubwa na kuacha takriban nyumba na maakazi milioni 3 bila ya umeme kwa mujibu wa tovuti ya umeme ya Marekani.

USA | Hurrikan Milton in Florida
Picha: Ricardo Arduengo/REUTERS

Kampuni za nishati ya umeme zinatoa huduma kwa takriban watu milioni 11.5 katika taifa hilo huku idadi inayoongezeka ya watu wakiendelea kukosa umeme kutokana na kiwango cha juu cha upepo, dhoruba kali na mvua kubwa ikiendelea kunyesha kutokana na athari za kimbunga Milton.

Haya yanajiri huku Rais Joe Biden akimshambulia mtangulizi wake kwa madai ya kueneza "uongo mkubwa" juu ya jinsi serikali yake ilivyolishughulikia suala la Kimbunga.

"Rais Trump ameongoza katika madai ya uongo. Madai kwamba mali zinachukuliwa. huo sio ukweli. Wanadai kwamba waathiriwa wa kimbunga wamepokea dola 750 pesa taslimu na zaidi. Wanasema pesa zinazohitajika kushughulikia majanga haya zinaelekezwa kwa wahamiaji. Acha sio ukweli na inatia hasira," alisema Trump.

Kimbunga Milton kimetuwa Florida na kinatajwa kuwa kikali na cha hatari zaidi, kikipiga kwa kiwango cha  daraja ya 3.