1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Milton chatuwa Florida

10 Oktoba 2024

Rais Joe Biden wa Marekani amemshambulia mtangulizi wake kwa madai ya kusambaza kile alichosema ni "uongo mkubwa" juu ya jinsi serikali yake inavyolishughulikia suala la Kimbunga Helene, huku Kimbunga Milton kikiwasili.

Joe Biden Florida
Rais Joe Biden wa Marekani akizungumzia vimbunga Helene na Milton vilivyopiga nchi yake.Picha: Tierney L. CrossPool/CNP/ZUMA Press Wire/IMAGO

Akizungumza kwenye Ikulu ya White House, amesema kauli ya Donald Trump zinakwenda kinyume na maslahi ya Marekani.

Trump na wasaidizi wake wanailaumu serikali ya Biden kwa kutokuchukuwa hatua muafaka kukabiliana na athari za Kimbunga Helene, ambacho kimelipiga na kuliathiri vibaya jimbo la North Carolina na kugharimu maisha ya watu 230.

Mgombea huyo urais kupitia chama cha Republican amesema utawala wa Biden na mshindani wake kwenye uchaguzi wa Novemba, Makamu wa Rais Kamala Harris, umeshindwa kuliko hali ilivyokuwa kwenye Kimbunga Katrina kilichouwa watu 1,392 mwaka 2005.

Kimbunga Milton ambacho tayari kimetuwa Florida kinatajwa kuwa kikali na cha hatari zaidi, kikiwa kimepandishwa kiwango chadi Daraja ya 3.