1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaChina

Kimbunga Saola chaelekea miji mikubwa ya kusini mwa China

Sylvia Mwehozi
1 Septemba 2023

Mamilioni ya watu katika eneo la kusini mwa China, wametafuta hifadhi wakati kimbunga Saola kikipiga kuelekea miji mikubwa ya Hong Kong na Shenzhen.

China Supertaifun Saola nähert sich Hongkong
Picha: Keith Tsuji/ZUMA Press Wire/picture alliance

Kimbunga hicho kimelazimu mamia ya safari za ndege kufutwa, kikipiga katika kasi ya upepo wa kilomita 210 kwa saa kuelekea Hong Kong, kimbunga Saola kinaweza kuwa mojawapo ya vimbunga vikali zaidi kulikumba jimbo la Guangdong.

Mamlaka tayari zilikuwa zimetoa tahadhari ya juu zaidi ya kimbunga hicho, ambacho vyombo vya habari vya serikali ya China  vilisema kitapiga katika maeneo ya pwani leo Ijumaa.

Kimbunga hicho kilisababisha maelfu ya watu kuhamishwa mapema wiki hii huko kaskazini mwa Ufilipino, lakini hakuna majeruhi wa moja kwa moja ambao wameripotiwa kufikia sasa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW