1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Bemba akataa matokeo ya uchaguzi, aweka pingamizi.

19 Novemba 2006

Jean-Pierre Bemba mgombea aliyeshindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo , jana alitoa pingamizi rasmi dhidi ya matokeo ya uchaguzi huo , ambao umempatia ushindi rais wa sasa Joseph Kabila.

Kuna idadi kadha ya matukio ya uendeaji kinyume uchaguzi huu na ambayo yamesababisha udanganyifu katika matokeo hayo , ambayo yameatangazwa na tume huru ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa ahadi zilizotolewa na mgombea Jean-Pierre Bemba , tumekuja katika mahakama kuu kupinga dhidi ya mapungufu haya , amesema Delly Sessanga, msemaji wa muungano wa umoja wa kitaifa unaoongozwa na Bemba.

Alikuwa Sessanga ambaye amewasilisha pingamizi hiyo dhidi ya matokeo ya uchaguzi kwa niaba ya Bemba , kiongozi wa zamani wa waasi ambae hivi sasa ni mmoja kati ya makamu watano wa rais katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na mmoja kati ya watu tajiri sana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW