1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Bemba anapinga matokeo ya uchaguzi wa rais

17 Novemba 2006

Jean-Pierre Bemba aliepambana na Joseph Kabila katika uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo amesema,hawezi kuyakubali matokeo ya uchaguzi yaliotangazwa.Amesema atatumia njia zote za kisheria kupinga matokeo hayo.Halmshauri Huru ya Uchaguzi imetangaza kuwa rais wa hivi sasa Kabila ameshinda kwa asilimi 58.05 na makamu wa rais Bemba amejinyakulia asilimia 41.95 ya kura zilizopigwa.Viongozi wa pande zote mbili walitoa mito ya kuwa na utulivu baada ya ghasia kuzuka karibu na nyumba ya Bemba mjini Kinshasa,tarehe 11 Novemba na kusababisha vifo vinne.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia amewasihi viongozi wa kisiasa nchini Kongo na wananchi,kupokea matokeo ya uchaguzi kwa utulivu na wajibu.Matokeo hayo ya uchaguzi yanapaswa kuidhinishwa na Mahakama Kuu ya Kongo,kabla ya Kabila kuweza kuapishwa kama rais mpya,tarehe 10 Desemba.