1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA : Bunge lapitisha katiba mpya

14 Mei 2005

Bunge la taifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hapo jana limepitisha rasimu ya katiba nchini humo kama sehemu ya mchakato wenye lengo la kurudisha utulivu katika nchi hiyo ya Afrika ya kati.

Katiba hiyo ambayo baadae itawasilishwa kwenye kura ya maoni ya taifa imepitishwa na wabunge 348 dhidi ya watano walioipinga na wanane hawakushiriki kupiga kura miongoni mwa wabunge 361.

Katiba hiyo ambayo tayari imeidhinishwa na senate baraza la juu la bunge inampa Rais uwezo kuanzia kumteuwa na kumuondowa madarakani waziri mkuu hadi kuvunja bunge.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW