1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa: Jeshi jipya la Kongo lawavua silaha waasi

20 Novemba 2003

Jeshi kipya la taifa nchini Congo, limeanza kuwavua silaha wapiganaji wa kigeni kwa mara ya kwanza nchini humo, ishara ambayo inaonyesha maendeleo katika utaratibu wa amani, walisema maafisa wa Umoja wa Mataifa hiyo jana. Kuweko kwa waasi kutoka nchi jirani, kumekuwa sababu kubwa ya kuchochea vita katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, kukisababisha uvamizi wa majeshi ya kigeni na hali isiyokuwa salama katika eneo la Afrika ya kati. Maafisa wa Umoja wa Mataifa walisema, jeshi la Congo lilianza kuwavua silaha kwa hiari wapiganaji 361, wengi wao kutoka Rwanda, Uganda, Sudan na Burundi na watasafirishwa kutoka mji wa magharibi Kikwit hadi kutio cha Kitona kandoni mwa bahari ya Atlantik.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW