1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Kinshasa kuwa bila silaha.

24 Septemba 2006

Viongozi wawili ambao wanawania kuchaguliwa katika wadhifa wa urais wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo baada ya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia katika muda wa miaka 40, jana Jumamosi wameahidi kuufanya mji mkuu wa nchi hiyo , Kinshasa, kutokuwa na silaha.

Maafisa wanaokaimu nafasi za rais wa sasa Joseph Kabila na hasimu wake Jean-Pierre Bemba , wametia saini hatua ya makubaliano, wakiahidi kupunguza idadi ya silaha zinazopatikana katika mji huo.

Jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, MONUC , limesema mara kwa mara kuwa lina wasi wasi juu ya idadi ya silaha zinazopatikana ovyo katika mitaa ya Kinshasa , nyingi kati yake zikiwa katika mikono ya makundi ya wanamgambo ambao wanamuunga mkono ama Bemba ama Kabila.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW