1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinshasa. Kipindupindu chaingia jeshini.

27 Agosti 2005

Maafisa wa afya wamesema leo kuwa kuzuka kwa kipindupindu miongoni mwa wanajeshi na familia zao mashariki ya Congo kumesababisha vifo vya zaidi ya watu 12 na wengine kadha kuwa wagonjwa.

Kampo Abu-Bakr wa shirika la afya la umoja wa mataifa WHO amesema ugonjwa huo ulioingia katika kambi ya jeshi upande wa kaskazini katika jimbo la Kivu , umesababisha watu 753 kulazwa hospitalini na wengine 19 wamekufa.

Msemaji wa umoja wa mataifa katika mji wa mashariki wa Goma , Jacqueline Chenard amesema kuwa wanajeshi hao na familia zao huenda wamekunywa maji yenye vijidudu vya ugonjwa huo kutoka katika ziwa Kivu licha ya tahadhari zilizotolewa na gavana wac jimbo hilo kuwa maji ya ziwa hilo yana maradhi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW