Kinshasa. Mahasimu nchini Congo waonywa.
2 Agosti 2006Matangazo
Mataifa makuu katika umoja wa mataifa yamewaonya leo mahasimu katika jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kutopanda mbegu ya hali ya wasi wasi miongoni mwa wapiga kura wakati wakingojea matokeo ya mwanzo ya uchaguzi mkuu wa vyama vingi.
Wanasiasa na vyombo vya habari vinapaswa kuepuka kutoa taarifa za awali za matokeo ya kura, iliyofanyika hapo Julai 30, imesema tume ya kimataifa inayosaidia hatua ya mpito katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Onyo hilo limekuja baada ya vituo vya televisheni vya watu binafsi vinavyomilikiwa na baadhi ya wagombea , hasa rais Joseph Kabila na hasimu wake mkubwa makamu wa rais Jean-Pierre Bemba kutangaza matokeo katika miji na vijiji, na kuieleza kama ni msimamo ulivyo nchi nzima.