1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Majeshi yaondolewa mji mkuu

23 Agosti 2006

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa vikosi vilivyo tiifu kwa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo vimekubali kuondoka katikati ya mji mkuu Kinshasa. Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Kinshasa na wawakilishi wa rais Kabila,makamu war ais Jean-Pierre Bemba,MONUC,EUFOR na wa kikosi cha polisi wa Ulaya nchini Kongo EUPOL mjini Kinshasa.Kamanda mkuu wa majeshi ya Ujerumani yalio sehemu ya vikosi vya Umoja wa Mataifa kulinda usalama nchini Kongo.Mapigano makali kati ya wafuasi wa Kabila na mpinzani wake wa kisiasa Bemba yalizagaa mjini Kinshasa tangu siku ya Jumapili,baada ya kutangazwa kuwa wagombea hao wawili watapambana katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais mwezi wa Oktoba.Si chini ya watu 5 waliuawa katika machafuko hayo.Wakati huo huo Umoja wa Ulaya umepeleka Kongo wanajeshi 250 wengine kuwasaidia kama wanajeshi 1,000 wa umoja huo na 17 elfu wa Umoja wa Mataifa kulinda usalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW